• Breaking News

  Nov 25, 2016

  Mchungaji Anthony Lusekelo Mzee wa Upako Akamatwa na Polisi

  Mchungaji Anthony Lusekelo
  Mchungaji Anthony Lusekelo maarufu Mzee wa Upako wa Kanisa la Maombezi anashikiliwa na Jeshi la Polisi jijini Dar es Salaam akituhumiwa kuafanyia fujo majirani zake, kuwatolea lugha isiyofaa na kufunga barabara.

  Tukio hilo lilitokea juzi asubuhi karibu na nyumbani kwa mchungaji huyo wilayani Kinondoni ambapo majira ya asubuhi Mzee wa Upako alifikia kwenye geti la jirani wake na kuegesha gari lake katikati ya barabara na kuanza kutoa maneno machafu kuwalenga majirani zake. Mzee wa Upako anadaiwa kufikia ahatua hiyo baada ya majirani zake pamoja na walinzi kumuita yeye ni mlevi na kuwa hafai kuwa mchungaji.

  Majirani wengine waliokuwa wakishuhudia tukio hilo walisema kuwa kitendo hicho kilikuwa ni cha kufedhehesha ukilinganisha na nafasi na heshima yake katika jamii. Imeelezwa kuwa hata baada ya watu kumtoa hapo, baada ya muda mfupi alirejea na kuendelea kuporomosha lugha hiyo kabla ya Polisi kufika na kumchukua.

  Jeshi la Polisi limeeleza kuwa litatoa taarifa rasmi kuhusu kukatwa kwa Mchungaji Lusekelo leo Ijumaa Novemba 25.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku