• Breaking News

  Nov 6, 2016

  Mengine yaibuka Marekani kuhusu mke wa Trump


  Shirika la habari la Associated Press linasema limepewa nyaraka zinazoonyesha kuwa mke wa Donald Trump, ambaye ni mzaliwa wa Slovenia, Melani, alifanya kazi bila kibali alipowasili mara ya kwanza nchini Marekani.


  Mwana mitindio huyo wa zamani aliwasili nchini Marekani mwaka 1996 na alipewa kibali cha kufanya kazi mwezi Agosti mwa huohuo.


  Lakini kulingana na nyaraka hizo alilipwa dola 20,000 kwa kushiriri maonyesho ya mitindo kabla ya kupata kibali kamili.


  Bwana Trump ametangaza msimamo mkali dhidi ya wahamiaji haramu wakati wa kampeni, na kuapa kuwa atawafukuza wale walio na historia ya uhalifu. Kampeni ya Trump haijatoa tamko lolote kuhusu madai hayo.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku