Nov 10, 2016

Mikopo ya Wanawake Hutumiwa na Waume zao Kwenye Anasa

Matokeo ya utafiti wa kuangalia changamoto za ufanyaji biashara kwa mwanamke Tanzania umebaini kuwa wanaume hutumia mikopo ya wake zao kwa matumizi mingine ikiwamo anasa na pombe.

Utafiti huo uliofanyika kati ya Julai 30 na Agosti 12 mwaka huu, umetolewa jana mbele ya wajasirimali wanawake nchini kupitia mkutano wa Chemba ya Wanawake wajasiriamali nchini.

Utafiti huo ulihoji wanawake 154,makundi tisa na maofisa wa taasisi zisizo za kiserikali katika kanda sita za Tanzania bara.

Mtafiti na mwasilishaji wa utafiti huo ,uliojikita kuchambua na kutoa mapendekezo ya kumwezesha mwanamke,Ndasile Chamkunde amesema zinahitajika juhudi ili kumsaidia mwanamke kuongeza uwezo wake kibiashara.

"Changamoto nyingine ni mchakato mgumu wa kusajili biashara zao, nusu ya waliohojiwa ndio  wamejisajili.” amesema

Amesema asilimia 75 wanauza katika soko la Afrika Mashariki ila asilimia 78 wanauza kwa muda tu, elimu yao ni chini ya kidato cha nne, na asilimia 48 wanategemewa na watu sita kupitia biashara zao, "amesema Chamkunde ambaye pia ni muhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha UDSM.Bonyeza HAPA Kudownload Application ya Udaku Special Blog Kwenye Simu Yako

Share:

0 maoni:

Post a Comment

Trending News

Copyright © Siasa Huru | Powered by Blogger Design by JK | Blogger Theme by JR