• Breaking News

  Nov 19, 2016

  Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Aliyetumbuliwa Ateuliwa Kuwa RAS Kagera

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua aliyekuwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) Bw. Diwani Athuman kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera.

  Kwa mujibu wa Taarifa ya Kurugenzi ya mawasiliano Ikulu, uteuzi wa Bw. Diwani Athuman unaanza mara moja.
  Wakati huo huo, Rais Magufuli amefanya uteuzi wa Wenyeviti wa Bodi katika taasisi tano za Serikali kama ifuatavyo.
  Kwanza, amemteua Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jaji Joseph Sinde Warioba kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA)  uteuzi ambao umeanza tarehe 16 Novemba, 2016.


  Pili, Rais Magufuli amemteua Dkt. Jones A. Kilimbe kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na Bw. Sylvester M. Mabumba kuwa Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) uteuzi ambao umeanza tarehe 17 Novemba, 2016.
  Aidha amemteua Prof. Patrick Makungu kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Uhandisi na Usanifu Mitambo (TEMDO) uteuzi ambao umeanza tarehe 16 Novemba, 2016.
  Pia, Rais Magufuli amemteua Bw. Martin Madekwe kuwa mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Fidia ya Ardhi uteuzi ambao umeanza tarehe 17 Novemba, 2016.
  Kadhalika, Rais Magufuli amemteua Prof. Raphael Tihelwa Chibunda kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Wakurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Viuatilifu vya Kitropiki Tanzania (TPRI) uteuzi ambao umeanza tarehe 17 Novemba, 2016.


  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku