• Breaking News

  Nov 18, 2016

  Mkuu wa Idara ya Upelelezi Ajiuzulu Marekani


  Mkuu wa idara ya upelelezi nchini Marekani James Clapper aliyekuwa akihudumu katika awamu ya uongozi wa rais Barack Obama ametangaza kujiuzulu.

  Clapper amekuwa afisa wa kwanza wa ngazi za juu serikalini kuwasilisha barua ya kujiuzulu kufuatia uteuzi wa rais mpya Donald Trump nchini Marekani.


  Clapper ametoa tangazo la kujiuzulu wakati zimesalia siku 64 kabla ya rais mteule Donald Trump kushika hatamu White House.


  Clapper alitangaza kuchukuwa hatua hiyo baada ya kufanya mkutano na wawakilishi wa baraza la usalama na upelelezi nchini humo.


  Akifahamisha kuwasilisha rasmi barua yake ya kujiuzulu usiku wa jana, Clapper aliarifu kuridhishwa na maamuzi yake aliyochukuwa.


  Hata hivyo Clapper hakutoa sababu ya kujiuzulu mapema licha ya kuhudumu katika wadhifa huo kwa kipindi cha miaka 6.


  Clapper mwenye umri wa miaka 75 alistaafu kama kamanda mkuu wa kikosi cha jeshi la angani la Marekani na kuwahi kuhudumu kama afisa mkuu wa idara ya ulinzi kati ya mwaka 1992-1995.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku