• Breaking News

  Nov 13, 2016

  Mmiliki wa Kampuni ya UDA Akanusha Kauli ya Halima Mdee Kuwa Aliuziwa Kampuni Kinyemela


  Kampuni ya Simon Group inayomiliki mabasi ya UDA na mradi wa mabasi yaendayo haraka kwa ubia na Serikali imekanusha vikali madai ya Mbunge wa Kawe, Halima Mdee kuwa kuwa kampuni hiyo iliuzwa kwake kinyemela.                                

  Akichangia hoja hivi karibuni bungeni Dodoma, Mdee alisema kampuni ya UDA haikuuzwa kihalali kwa Simon Group Ltd, Waziri husika hakuridhia kihalali uamuzi wa Baraza la jiji, UDART iliuzwa kinyemela na SGL ilotumia rasilimali za UDA kupata mkopo wa kuendesha Udart.                   

  Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam, Msemaji wa SGL, Deus Bugaywa alisema madai hayo siyo ya kweli.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku