• Breaking News

  Nov 18, 2016

  Moi Yapambana Kumpatia tiba Kijana Mwenye Urefu wa futi 7.4

  Taasisi ya Mifupa Muhimbili (Moi) inaendelea kutafuta ufumbuzi wa kutibu tatizo la nyonga linalomkabili Baraka Elias, ambaye upasuaji wake umekuwa mgumu kufanyika kutokana na kukosekana vifaatiba vinavyolingana na urefu wa mifupa yake.

  Baraka mwenye urefu wa futi 7.4 alipata matatizo ya nyonga Aprili, baada ya kuanguka akiwa nyumbani kwake Mbinga mkoani Ruvuma.

  Awali, alipelekwa hospitali ya Peramiho lakini ilishindikana kumtibu na ndipo alihamishiwa Moi ambako nako ilishindikana kutokana na mifupa yake kuwa mirefu kupita kiasi.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku