• Breaking News

  Nov 8, 2016

  Muhimbili Watoa Tamko Kuhusu Kifo cha Joseph Mungai...Wadai Hakuwa Amelazwa Hospitalini Hapo


  Taarifa ambazo zimeripotiwa jioni ya November 8 2016 zimesema kuwa aliyewahi kuwa Waziri wa Elimu Tanzania, Joseph Mungai amefariki dunia huku taarifa za awali zikidai kuwa alianza kwa kutapika mfululizo, familia imedai kuwa tatizo hilo limemkuta baada ya kudaiwa kula kitu kibaya.

  Taarifa za kifo zilizothibitishwa na mkuu wa kitengo cha mawasiliano ya umma Hospitali ya Muhimbili, Aminiel Bubwerwa Aligaesha amesema wamethibitisha kifo chake ila hakuwa amelazwa hospitalini hapo.

  hakuwa amelazwa hospitali ya Taifa Muhimbili, sisi tumepokea mwili wake, amekuja akiwa ameshakufa na sisi tumepokea mwili wake katika idara yetu ya magonjwa dharura na madaktari wetu wakathibitisha kifo chake na kupeleka mwili wake kwenye chumba cha kuhifadhi maiti’

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku