Nov 17, 2016

Mwigulu Aonyesha Mfano kwa Wadaiwa Bodi ya Mikopo, Aanika Marejesho ya Mkopo wake


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba ameonyesha mfano bora kwa wadaiwa wa Mikopo ya Elimu ya Juu baada ya kuanika nyaraka za marejesho yake ya fedha alizokopeshwa na serikali kupitia akaunti yake ya Facebook na kuwataka Watanzania kurejesha mikopo kwa manufaa ya wengine.

Waziri Nchemba ametoa ujumbe huo ikiwa ni siku chache tangu Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu kutoa siku 30 kwa wadaiwa sugu wa mikopo hiyo kurejesha mikopo yao.

Mhe. Mwigulu amewataka wadaiwa kulipa mikopo hiyo ili Watanzania wengine nao wapate fursa ya kusoma huku akisema kuwa amelipa deni lake kuanzia mwaka 2007 hadi mwaka 2013.

Katika nyaraka hizo inaonyesha Waziri Nchemba alitumia muda wa miaka sita kulipa deni lake la Tshs 2,153,400 kwa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu.

Huu ndiyo ujumbe aliyouandika Mhe. Mwigulu kwenye akaunti yake ya FacebookBonyeza HAPA Kudownload Application ya Udaku Special Blog Kwenye Simu Yako

Share:

0 maoni:

Post a Comment

Trending News

Copyright © Siasa Huru | Powered by Blogger Design by JK | Blogger Theme by JR