• Breaking News

  Nov 28, 2016

  Mzee wa Miaka 86 Jela Kwa Kufanya Mapenzi na Bintiye

  MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi wa Wilaya ya Urambo imemhukumu kwenda jela miaka 30 mzee mwenye umri wa miaka 86 kwa kosa la kufanya mapenzi na mahalimu wake (binti yake wa kumzaa).

  Alipewa adhabu hiyo na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya wilaya hiyo, Hassan Momba ni Mzee Nasspra Kalmati maarufu kwa jina la Mbavu Mbili baada ya kumtia hatiani kwa kufanya mapenzi na binti yake mwenyewe wa umri wa miaka minane.

  Hakimu Momba alisema kwa kuzingatia ushahidi uliotolewa na upande wa mashitaka imethibitika pasipo shaka kwamba mshitakiwa ametenda kosa hilo kwa makusudi.

  Mshitakiwa Mbavu Mbili ambaye alikamatwa Oktoba mwaka huu, inadaiwa kuwa alitenda kosa hilo la kinyama kati ya Januari na Oktoba 20, mwaka huu kinyume cha Kifungu namba 158 (1) (a) cha Makosa ya Jinai.

  Awali, upande wa mashitaka ukiongozwa na Mkaguzi wa Polisi, Philibert Pimma ulidai kuwa kati ya Januari 2016 hadi 0ktoba 20, mwaka huu katika tarehe tofauti tofauti mshitakiwa alikuwa akifanya ngono na binti yake (jina linahifadhiwa).

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku