• Breaking News

  Nov 9, 2016

  Mzungu Amlazimisha Mwafrika Kuingia Kwenye Jeneza ili Amuue

  Johannesburg, Africa Kusini
  Hisia kali zimetolewa mitandaoni baada ya mwanamume mzungu kuonekana akimwingiza mwanamume mweusi kwenye jeneza kwa lazima huku akitishia kumchoma akiwa hai

  Video iliyosambazwa mitandaoni ilionyesha tukio hilo ambalo wengi wanasema ni dhihirisho la jinsi ukandamizaji wa Waafrika weusi bado unaendelezwa nchini humo

  Kwenye video hiyo ya sekunde 20, Mwanamume mweusi aliyeingizwa kwenye jeneza anasikika akilia huku mzungu anayeaminika ni mkulima akifunga jeneza hilo kwa lazima

  Anasikika akimwambia "Ingia ndani... ninataka kumwaga petroli"

  Mwingine ambaye haonekani lakini anaaminika ndiye aliyekuwa akinasa video hiyo anasikika akitishia kuingiza nyoka ndani ya jeneza hilo kama kijana huyo mweusi ataendelea kujaribu kujinasua

  Kumekuwa na malalamiko ya Waafrika weusi kuhusu ubeberu nchini humo ambapo hivi majuzi wanafunzi wa vyuo vikuu waliandamana kutaka sanamu za kibeberu zibomolewe katika vyuo vyao

  Matukio mengine ambapo waafrika weusi walilazimishwa na wazungu kunywa mikojo yao, pia yamewahi kuripotiwa.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku