Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta a.k.a 'Sama Goal' amesema yupo katika wakati mgumu na anahitaji kupambana kurudisha nafasi yake katika klabu ya KRC Genk.

Katika siku za karibuni Samatta amekuwa akipangwa dakika za mwisho mwisho za mchezo kutokana na mshindani wake wa namba, Nikolaos Karelis kufanya vizuri zaidi yake.

“Tunayecheza naye nafasi moja anafanya vizuri, yuko kwenye fomu nzuri anafunga karibu kila mechi, kwa hiyo anastahili kuanza mechi,” amesema Samatta.
       
Makali ya Samatta yalianza kupungua baada ya kuumia kwenye mchezo wa Europa League dhidi ya Rapid Wien ya Austria Septemba 15, mwaka huu Genk ikishinda 3-2 ambapo siku hiyo, Samatta alishindwa kuendelea na mchezo baada ya kuumia na kutoka dakika ya 78, huku nafasi yake ikichukuliwa na Mbelegiji huyo.


Post a Comment

 
Top