• Breaking News

  Nov 15, 2016

  Nchi Nyingine ya Afrika Yatangaza Kujitoa ICC Baada ya Madai kuwa Mahakani Hiyo Inanyanyasa Nchi za Afrika


  Fatou Bensouda ambaye ni kiongozi wa mashtaka wa mahakama hiyo ni raia wa Gambia

  Gambia imetangaza nia yake ya kuwa taifa la tatu barani Afrika kujitenga na mkataba wa Roma uliounda mahakama ya kimataifa ya jinai ICC.

  Tayari Burundi na Afrika Kusini zimetangaza kujitoa kutoka kwenye mahakama hiyo.

  Waziri wa mawasiliano ya taifa hilo,Sheriff Bojang, anasema mahakama hiyo inatumika kuwanyanyasa Waafrika.

  Fatou Bensouda, mwendesha mshataka wa mahakama hiyo ni raia wa Gambia.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku