• Breaking News

  Nov 17, 2016

  Picha: Waandamanaji Brazil waingia kwa nguvu Bungeni

  Waandamanaji nchini Brazil ambao wanataka yafanyike mapinduzi ya kijeshi, wameingia kwa nguvu katika majengo ya bunge kwenye mji mkuu Brasilia.

  Takriban waandamanaji 40 walipambana na walinzi na kufanikiwa kuingia katiak jukwaa la bunge wakati kikao kilikuwa kikianza siku ya Jumatano.

  Wakikemea ufisadi serikalini, waandamanaji hao walitaka kurejea kwa utawala wa kijeshi, ambao uliitawala nchi kati ya mwaka 1964 hadi 1985.


  Mjini Rio de Janeiro polisi walirusha vitoa machozi kwa wafanyikazi wa umma waliokuwa wakipinga kupunguzwa kwa mishahara

  Waandamanaji hao waliwashinda nguvu walinzi na kuvunja mlango wa kuingia bunge ambapo walipiga mayowe na kuimba wimbo wa taifa.

  Iliwachukua polisi muda wa saa kuwazingira waandamanaji hao.

  Baadaye msemaji wa Rais Michel Temer alilaani maandamano hayo na kusema kuwa yalikuwa ni ukiukaji wa uwepo wa demokrasia.

  Wengi wa waandamanaji mji Rio walikuwa ni wafanyakazi wa umma

  Imani ya watu kwa mashirika ya umma nchini Brazil imeathiriwa na ufisadi mkubwa pamoja na kuondolewa madarakani kwa rais Dilma Rousseff.

  Bwana Temer alikuwa makamu wa rais kabla ya kuwa rais kufuati kutimuliwa kwa Rousseff.

  Brazil ni moja ya nchi za Amerika ya Kusini ambapo jeshi lilipindua serikali zilizochaguliwa kidemokrasia miaka ya sitini na sabini.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku