Nov 21, 2016

Polisi watibua saa 48 za Maalim Seif

Lindi. Saa 48 za Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad zimekuwa chungu baada ya  kushindwa kufanya mikutano yake miwili mkoani Lindi baada ya polisi kuizuia kwa sababu za kiusalama.

Hii ni mara ya pili kwa  Maalim kukwama kufanya mikutano yake baada ya juzi polisi kumzuia tena asifanye mkutano wake mpaka pande mbili zinazosuguana ndani ya chama hicho zitakapokaa na kukubaliana.

Maalim Seif ambaye alikuwa afanye mkutano wake wa kwanza katika eneo la Mnazi Mmoja mkoani Lindi na wa pili Lindi mjini, yote ilishindikana.

Kamanda wa Polisi mkoa ni Lindi, Renata Mzinga alipoulizwa sababu za kuzuia mikutano hiyo alijibu kwa kifupi tu kuwa ni sababu za kiusalama.

Bonyeza HAPA Kudownload Application ya Udaku Special Blog Kwenye Simu Yako

Share:

0 maoni:

Post a Comment

Trending News

Copyright © Siasa Huru | Powered by Blogger Design by JK | Blogger Theme by JR