• Breaking News

  Nov 15, 2016

  Prof Lipumba: Kuna Hali Mbaya CUF, Fedha za Ruzuku Hazitoki Sababu ya Mgogoro Ndani ya Chama

  Prof Ibrahim Haruna Lipumba yupo Tabora.Huko ndio kwao,kijiji cha Ilolangulu ambacho ni kilomita kadhaa kutoka Tabora mjini.Leo Prof alikuwa na wanachama wa CUF Mkoa wa Tabora akiwasisitiza kuwa kwa sasa ndani ya CUF hali ni ngumu sana.

  Prof anaseema hata yeye anasafiri kwa shida na taabu sana,sbb mgogoro ndani ya CUF umefanya ruzuku ya chama izuiliwe mpaka pale mgogoro utakapotatuliwa.Prof anawaambia wananchi na wanachama wa Tabora,ameamua kurudi kwenye Chama na kutengua barua yake baada ya kuona chama kinaenda kombo...anaomba wana Tabora wamuunge mkono,maana katika ngome za CUF huku Tz Bara,basi Tabora ndio maeneo yake.

  Naye Mwanachama aliyesimamishwa Abdul Kambaya anasema CUF ni ya Tanzania bara na si Zanzibar,maana waanzilishi wake kina Mapalala na Mzee Mloo ndio waliohangaika na CUF,wakati kule Znz kulikuwa na KAMAHURU kwa ajili ya Wazanzibar,sasa haiwezekani CUF ya Tz Bara iliyowaalika tu watu kama kina Maalim Seif toka Znz waje bara na kutaka kutawala siasa za CUF.Kambaya anasema Maalim Seif na watu wake waende kuhuisha KMAHURU yao na waachie CUF kwa Watanzania Bara wanaojua uchungu wake.

  Amesisitiza kuwa Tabora ni ngome ya CUF miaka mingi,lkn ajabu uchaguzi wa mwaka jana mji mzima ulijaa bendera za CHADEMA.

  Prof amemalizia kwa kuwaomba wana Tabora kumuunga mkono ili kukirudisha chama cha CUF mikononi mwa wananchama wa Tanzania bara.Haya ndio maneno ya "Bwana Yule" leo,huko Mboka Manyema

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku