• Breaking News

  Nov 22, 2016

  Profesa Ndalichako: Adhabu Shuleni zisihusishwe na Siasa

  Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako amesema siasa inatakiwa kuepukwa katika itoaji wa adhabu shuleni.

  Akizungumza leo (Jumanne) wakati wa kufungua mdahalo wa wanafunzi wa sekondari mbalimbali za jiji Dar es salaam, Profesa Ndalichako amesema  mwanafunzi anatakiwa kuadhibiwa baada  baada ya bodi ya shule  kujadili na kufanya maamuzi.

  Waziri huo amewataka wanafunzi kuwa makini kwenye matumizi ya mitandao ya kijamii kwa sababu katika mitandao hiyo kuna  mijadala na picha zinazokiuka maadili ya nchi.

  Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Binto Musa Binto amesema tatizo kubwa linalosababisha mmomonyonyoko wa maadili katika jamii ni kukosa uwezo wa kichambua athari mbaya na nzuri zinazotokana na utandawazi.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku