• Breaking News

  Nov 22, 2016

  Rapper Kanye West Alazwa Hospitalini, Akatisha Show zake


  Rapper Kanye West amelazwa katika hospitali huko jijini Los Angeles. Hatua hiyo imekuja baada ya kukatisha show zilizokuwa zimesalia za ziara yake ya Saint Pablo kutokana na kukabiliwa na uchovu.

  Kwa mujibu wa NBC News, Kanye alipelekwa hospitali baada ya polisi kupigiwa simu ya dharura. Wiki hii rapper huyo ametengeneza vichwa vya habari kwa kauli tata alizozitoa wakati wa show zake mbili zilizopita ikiwemo kuwadiss Jay Z na Beyonce na kumfagilia Donald Trump.

  Kutokana na kukatisha show zilizokuwa zimesalia, West atapata hasara ya zaidi ya dola milioni 10.

  Familia yake ipo kwenye wakati mgumu kwa sasa. Mwezi uliopita, mkewe Kim Kardashian, alivamiwa kwa mtutu wa bunduki na kuporwa mali huko Paris, Ufaransa.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku