• Breaking News

  Nov 25, 2016

  Ruge Mutahaba wa Clouds FM Afunguka Kuhusu Ugomvi wake na Mwanamuziki Lady Jay Dee

  Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Live, Ruge Mutahaba leo amefanya mahojiano na Clouds Fm na kuzungumzia kuhusu muziki wa Tanzania.

  Miongoni mwa mambo mengi aliyoyazungumzia ni kuhusu tofauti kati yake na mwanamuziki Judith Wambura maarufu Lady JayDee na kueleza ni kitu gani hasa kilisababisha wasielewane na kufikia hatua kuwa Clouds Fm kutocheza tena nyimbo za msanii huyo.

  Akijibu swali lililoulizwa na mtangazaji B Dozen, kuwa ni kwanini yeye na Lady JayDee hawana maelewano mazuri. Mutahaba alisema kuwa chanzo cha kutokuelewana  ni baada ya mwanamuziki huyo kuchukua maeneo aliyodai kuwa ameambiwa Ruge Mutahaba na Joseph Kusaga wamesema kuhusu yeye.

  Sauti: Mkurugenzi wa Clouds, Ruge Mutahaba aeleza sababu ya Ruby kujitoa THT
  Mutahaba alisema baada ya maeno hayo kusambaa, Lady JayDee alimtaka Ruge na Clouds Media kutocheza nyimbo zake wala kutaja jina lake katika vituo vyao vyote. Baada ya kupokea taarifa hiyo basi nao walitekeleza kuwa kwanzia siku hiyo hawakuwa wakicheza nyimbo wala kutaja jina lake, alisema Ruge.

  Ugomvi huo uliendelea na Lady JayDee aliandika waraka uliobeba kichwa cha “Wosia wangu ikitokea nimetangulia kufa kabla ya Ruge na Kusaga,” ambao ulichapishwa kwenye gazeti na tovuti yake akizungumza mambo mengi kuhusu viongozi hao wa Clouds Media Group.

  Ruge na Kusaga walifungua kesi mahakamani kuhusu waraka huo ulioandikwa wakimtuhumu msanii huyo kuwa amewakashifu na Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni ilimuamuru Lady JayDee awaombe msamaha.

  Lady JayDee matatani, mahakama yamuamuru amuombe Ruge msamaha
  Akijibu swali kama yupo tayari kumsamehe LadyJayDee, Ruge alisema kuwa ndiyo yupo tayari na angefurahi kama angepata nafasi ya kuzungumza naye. Kuhusu kucheza nyimbo za mwanamuziki huyo, Ruge alisema wao ndio waliozuia tusicheze nyimbo zao, hivyo ikifika siku wakibadilisha msimamo wao na kutaka tucheze, basi tutacheza.

  Mbali na kuzungumzia ugomvi wake na Lady JayDee, Mutahaba amezungumzia pia mambo mengi kuhusu muziki wa Tanzania na ni kitu gani watanzania wasanii wa Tanzania wanatakiwa kufanya ili kuweza kuuinua muziki kwenda kimataifa. Aidha, pia Mutahaba alizungumzia changamoto nyingi ambazo zinawafanya wasanii mbalimbali kwenda kufanyia video nje ya nchi wakati Tanzania kuna maeneo mazuri zaidi pamoja na mambo mengine kuhusu maisha yake binafsi.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku