• Breaking News

  Nov 3, 2016

  Scorpion Apandishwa Tena Kizimbani

  KWA mara ya nne , Salum Njwete ‘Scorpion’ ambaye anadaiwa kumtoboa macho Said Ally amepandishwa  kizimbani katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala, Dar na kesi yake kusogezwa mbele.

  Scorpion alipandishwa kizimbani mbele ya Hakimu Flora Haule ambapo kesi yake ilitajwa na kupangiwa tarehe nyingine kutokana na upelelezi kutokamilika.

  Kesi ya Scorpion ambayo inavuta hisia za watu wengi ambao wamekuwa wakijaa mahakamani hapo wakiwemo ndugu zake na wale wa upande wa pili wa Said, imepangwa kutajwa tena Novemba 16, mwaka huu.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku