BUNGENI: Serikali yaitaka sekta binafsi kuwekeza katika kinywaji aina Gongo ili kurasimisha kinywaji hicho na kiwe salama kwa matumizi.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Viwanda na Biashara, Charles Mwijage alipokuwa akijibu maswali ya Wabunge

Baadhi ya Wabunge wamesema kinywaji hicho ni kinywaji rasmi kwa baadhi ya makabila, hivyo Serikali isizuie wananchi kutengeneza bali ikirasimishe ili iweze kukusanya kodi.


Post a Comment

 
Top