• Breaking News

  Nov 16, 2016

  Shein Asaini Sheria ya Mafuta na Gesi Kwa Mbwembwe

  Licha ya Wanasheria kumsihi Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Dk Ali Mohammed Shein asisaini Sheria ya Mafuta na Gesi, kiongozi huyo amepuuza wito huo na kufanya hivyo kwa mbwembwe katika tukio lililotangazwa moja kwa moja kwenye televisheni na redio kutoka Ikulu.

  Lilikuwa ni tukio la kipekee kwa kuwa historia haionyeshi kama Rais wa Zanzibar aliwahi kusaini sheria mbele ya viongozi mbalimbali wa chama na Serikali, huku likionyeshwa moja kwa moja kwenye televisheni.

  Kuonyesha kwamba utiaji saini huo una baraka za Serikali ya Muungano, tukio hilo lilihudhuriwa na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo.


  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku