Nov 3, 2016

Sirudi Bongo Movie hadi wezi wakamatwe - Dr. Cheni

Msanii nguli wa filamu Tanzani Dkt. Cheni amesema hatarajii kutoa movie hivi karibuni mpaka wezi wa kazi zao kwa kuzisambaza bila vibali watakapokamatwa.

Pia Dkt. Cheni akiongea na eNewz ameiomba serikali iwekeze katika tasnia ya bongo movie kwa kuwa imewabeba vijana wengi sana nchini ambao hawana ajira na walio na ajira hivyo serikali ikiweza na kusaidia katika kukomesha wizi itatoa ajira kwa vijana wengi zaidi

Hata hivyo Dkt. Cheni amesema wanaosambaza kazi zao ndiyo wezi wa kazi zao japokuwa taarifa zinaweza zikawa hazijaifikia serikali lakini watajitahidi kutoa ushirikiano kwa Mh.Nape Nnauye ili kuweza kuwakamata wezi kirahisi zaidi na kuokoa tasnia hii.

Bonyeza HAPA Kudownload Application ya Udaku Special Blog Kwenye Simu Yako

Share:

0 maoni:

Post a Comment

Trending News

Copyright © Siasa Huru | Powered by Blogger Design by JK | Blogger Theme by JR