• Breaking News

  Nov 16, 2016

  Staili Nyingine yaibuka Sakata la Godbless Lema

  Sakata la mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema dhidi ya vyombo vya dola limeendelea kwa staili nyingine ya kushindwa kumpeleka mahakamani jana kujibu tuhuma za uchochezi dhidi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo.

  Lema amesota rumande kwa siku 13 ambazo ni sawa na saa 312.

  Mbunge huyo amekuwa kwenye msukosuko wa kisheria na Jamhuri iliyomshtaki kwa tuhuma za kutoa maneno ya uchochezi na mapema wiki hii alipewa dhamana ambayo haikufanikiwa baada ya mawakili wa Serikali kuwasilisha taarifa ya kusudio la kukata rufaa kabla ya hakimu kuruhusu kutekelezwa kwa utaratibu wa dhamana.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku