• Breaking News

  Nov 22, 2016

  Taarifa ya Mugabe Kustaafu Urais Zimbabwe


  Kwa mara ya kwanza rais mkongwe wa Zimbabwe Robert Mugabe adokezea kuhusu kustaafu kwake .

  Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na gazeti linalomilikiwa na serikali la Sunday Mail ni kuwa  rais alisema "Nitastaafu ipasavyo."

  Rais Mugabe alisema hayo mwishoni mwa wiki katika mkutano na washirika wa vita mjini Harare .

  Hata hivyo neno 'Ipasavyo' kama alivyotumia katika kauli yake halikueleweka vizuri.

  Vile vile Robert Mugabe ameripotiwa kusema kuwa naamini kuwa ameshinda serikali za Uingereza na Marekani .

  Wakati huo huo televisheni ya habari za taifa ya ZBC ilitangaza kuwa mikoa mingi ya chama cha ZANU PF imeunga mkono Robert Mugabe kuwa mgombea wa urais katika uchaguzi wa mwaka 2018 .

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku