• Breaking News

  Nov 18, 2016

  Tanesco Yapingwa Kuongeza Bei ya Umeme

  Wakati wadau wa umeme jijini Dar es salaam wakisubiri wiki ijayo kutoa maoni kuhusu pendekezo la Tanesco kuongeza bei ya nishati hiyo kwa asilimia 18.19, wenzao kwenye kanda nne wamepiga hatua hiyo.

  Msimamo huo umetolewa kwenye mikoa ya Arusha, Mwanza, Dodoma na Mbeya ambako vikao vya kukusanya maoni ya wadau vimefanyika chini ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati (Ewura).

  Naibu Mkurugenzi Mkuu (Usafirishaji Umeme) wa Tanesco, Kahitwa Bishaija alisema shirika hilo limelazimika kuwasilisha ombi la kupandisha bei ili kumudu gharama za uzalishaji, usafirishaji, usambazaji na kuboresha huduma kwa wateja.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku