• Breaking News

  Nov 8, 2016

  TANZIA: Mwenyekiti wa Klabu ya Azam Afariki Dunia


  TANZIA: Mwenyekiti wa Klabu ya Azam, Mzee Said Mohamed Abeid, amefariki dunia akiwa kwenye matibabu katika Hospitali ya Aga Khan jijini Dar.

  Mzee Said Mohamed, atakumbukwa kama mmoja wa nguzo muhimu kwenye mafanikio ya klabu ya Azam FC tangu kuanzishwa kwake miaka takribani nane iliyopita.

  Chini ya uongozi wake kama mwenyekiti wa Azam FC, aliiongoza klabu hii kunyakuwa mataji mbalimbali makubwa na kwa mafanikio, ikiwemo taji la Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Ligi Kuu Tanzania Bara na Kombe la Mapinduzi mara mbili pamoja na Ngao ya Jamii.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku