• Breaking News

  Nov 24, 2016

  Tathmini ya Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi Juu ya Utendaji Kazi wa Rais Magufuli

  Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Alhaji Dkt. Ali Hassan Mwinyi leo ametoa tathmini yake ya mwaka mmoja wa uongozi wa Rais Dkt John Pombe Magufuli tangu alipoingia madarakani Novemba 5, 2016.

  Mzee Mwinyi amesema kuwa Rais Dkt Magufuli amefanyakazi kazi kubwa sana ndani ya mwaka wake mmoja ambapo amewataka watanzania kuendelea kumuunga mkono kwa kipindi chake chote kilichosalia.

  Akiongea na waandishi wa habari leo baada ya kufanya mazungumzo na Rais Dkt Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam, Mzee Mwinyi alisema kuwa Rais Dkt Magufuli amefanya kazi kubwa sana kwa mwaka mmoja kuliko waliyofanya watangulizi wake wote katika vipindi vyao vyote walivyokuwa madarakani.

  Rais amefanya mengi kwa kukabiliana na rushwa ambayo imekuwa ni changamoto kubwa tangu enzi za Mwalimu Nyerere. Sisi tulikuwa tuna ponda ponda, lakini kwa mwaka mmoja wake yeye ameleta Tsunami, na mimi nalifurahia hilo, alisema Mzee Mwinyi.

  Kwenye kuunda serikali, Mzee Mwinyi amempongeza rais kwa kuteua wachapakazi huku akisema kuwa ili serikali iweze kuendelea ni lazima kuwa na watumishi wachapakazi ambao watamsaidia rais kutekeleza majukumu.

  Aidha, Mzee Mwinyi alisema kuwa wandishi wa habari wamsaidie Rais kueleza habari ambazo zinapotoshwa katika jamii kwani mambo mengi yanayoelezwa si ya kweli.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku