• Breaking News

  Nov 10, 2016

  Time ya Simba Yachezea Kipigo Kitakatifu Mbeya....


  Maafande wa Tanzania Prisons wameetonesha kidonda cha ‘mnyama’ baada ya kumtandika bao 2-1 kkwenye mchezo wa ligi kuu Tanzania bara uliochezwa kwenye uwanja wa Sokoine, Mbeya.

  Jumapili November 6, African Lyon walikata utepe wa vipigo kwa Simba baada ya kuibuka na ushindi wa goli 1-0 kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam mchezo ambao ulikuwa kwanza kwa Simba kupoteza tangu kuanza kwa ligi msimu huu.

  Simba ndio walikuwa wa kwanza kufunga bao dakika ya 44 likifungwa kwa kichwa na Jamal Mnyate aliyeunganisha krosi ya Shiza Ramadhani Kichuya

  Bao hilo liliipa Simba uongozi wa hadi kipindi cha kwanza kinamalizika.

  Kipindi cha pili Tanzania Prisons walirejea vyema na kufanikiwa kupata bao la kusawazisha kupitia kwa Victor Hangaya ikiwa ni dakika tatu tangu kuanza kwa kipindi cha pili. Hangaya aliungasha pasi safi ya Kimenya ambaye ni beki wa kulia wa Tanzania Prisons.

  Wakati Simba wakipambana kutafuta bao la pili, Prisons wakaongeza goli la pili na kuwa mbele kwa bao 2-1 dhidi ya Simba bao likifungwa dakika ya 63 na Victor Hangaya.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku