• Breaking News

  Nov 17, 2016

  Tundu Lissu: Mkuu wa Wilaya ni Mkuu wa Majeshi wilayani kwake?

  Anaandika Tundu Lissu..

  Mkuu wa Wilaya ni Mkuu wa Majeshi wilayani kwake??? Huu ujinga unatoka wapi??? Ni sheria ipi inayomfanya Mkuu wa Wilaya Mkuu wa Majeshi ya Wilaya??? Mkuu wa Wilaya ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya kwa mujibu wa Sheria ya Baraza la Usalama la Taifa. Je, uenyekiti huo unamfanya Mkuu wa Majeshi??? Rubbish!!! Mkuu wa Wilaya ana mamlaka ya kipolisi (police powers of arrest in cases where there are no police officers present) kwa mujibu wa Sheria ya Tawala za Mikoa. Je, mamlaka hayo ya kipolisi yanamfanya DC kuwa Mkuu wa Majeshi ya Wilaya? Rubbish!!! Tunawakweza wakubwa hawa kwa kuwapa mamlaka wasiyokuwa nayo. Matokeo yake wanavimbisha vichwa na kuanza kutumia nguvu na mabavu dhidi ya wananchi kinyume kabisa na sheria. Mamlaka halali waliyonayo MaRC na maDC kwa mujibu wa Sheria hizo mbili ni very limited na yana masharti mengi. Kuvaa military uniforms na kubeba silaha za kijeshi wakati yeye sio Mwanajeshi ni kinyume cha sheria. Anatakiwa kukamatwa na kuchukuliwa hatua stahiki za kisheria. Ukuu wake wa Wilaya haumpi kinga yoyote kisheria. Kama hatakamatwa na kushtakiwa haitakuwa ni kwa sababu alichofanya ni sawa bali ni kwa sababu ya culture of impunity (utamaduni wa kuvunja sheria) iliyowajaa watawala wetu.

  Sheria ipi ya Tanzania hii inayosema majeshi au vyombo vyote vya usalama viko chini ya Mkuu wa Wilaya??? Mapolisi wote wilayani wako chini ya OCD, sio DC. Magereza wote wilayani wapo chini ya DPO, sio DC. Migambo nao hawako chini ya DC bali wako chini ya Kamanda wa Mgambo wa Wilaya. DC ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama tu. Sio Kamanda Mkuu wa kikosi chochote kilichopo wilayani. Kazi yake ya uenyekiti ni purely political coordination, sio operational. Hii habari iliyozoeleka kuwa DC ni Rais wa Wilaya au Mkuu wa vyombo vya ulinzi na usalama ni political nonsense.

  Source:Henry Kilewo

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku