Nov 6, 2016

Umeipata hii ya Mmiliki wa Facebook kushtakiwa nchini Ujerumani?


Mahakama moja mjini Munich nchini Ujerumani imefungua kesi dhidi ya muasisi wa mtandao wa kijamii wa Facebook, Mark Zuckerberg kwa kuchochea hisia za chuki.

Muasisi wa mtandao wa kijamii wa Facebook, Mark Zuckerberg

Jarida la habari la Ujerumani Der Spiegel limeripoti kuwa kesi hiyo iliwasilishwa na wakili mmoja wa mjini W├╝rzburg, anayeutuhumu mtandao wa Facebook kwa kuruhusu wito wa mauaji, vitisho vya machafuko, kukanusha mauaji ya Wayahudi, miongoni mwa mambo mengine.


Sheria zinazodhibiti maneno ya chuki nchini Ujerumani ni kali, ambapo ishara za Kinazi na propaganda za kibaguzi zimepigwa marufuku kabisa.


Mtandao huo wa kijamii umekuwa ukishutumiwa mara kwa mara kwa kuchukua muda mrefu kuondoa habari zenye maudhui yanayokiuka sheria kutoka kwa tovuti yake.


Bonyeza HAPA Kudownload Application ya Udaku Special Blog Kwenye Simu Yako

Share:

0 maoni:

Post a Comment

Trending News

Copyright © Siasa Huru | Powered by Blogger Design by JK | Blogger Theme by JR