• Breaking News

  Nov 6, 2016

  Umemsikia Lipumba kuhusu njia anayotaka CUF Kumaliza Mgogoro wao?


  M/Kiti wa chama cha wananchi CUF Prof. Ibrahim Lipumba amesema Mgogoro wa uongozi uliokikumba chama hicho unaweza kumalizwa kwa mazungumzo na kumtaka katibu Mkuu wa Chama hicho Maalim Seif Shariff Hamad kukaa pamoja ili kukinusuru chama hicho


  Prof.Lipumba ametoa wito huo wakati akiwa katika mikutano ya ndani na viongozi wa matawi, mashina na wanachama wa chama hicho katika wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani na kuwataka wanachama hao kujenga mshikamano ili kukinusuru chama hicho.


  Amesema tangu chama hicho kiingie katika mgogoro wa uongozi baada ya yeye kufuta azma yake ya kujiuzulu na kuvurugika mkutano mkuu maalum, baadhi ya wanachama wamegawanyika huku wengine wakiwa katika sintofahamu dhidi ya Mgawanyiko unaoendelea ndani ya chama hicho.


  Chama cha wananchi Cuf kimekumbwa na Mgogoro wa Uongozi tangu Prof.Lipumba kutengua Uamuzi wake wa kujiuzuru ndani ya chama hicho ambapo umesababisha mgawanyiko na kusababisha shughuli mbali mbali za chama zikiwemo za kuimarisha chama kusuasua.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku