• Breaking News

  Nov 26, 2016

  Ummy Mwalimu Azuia Kuhamisha Vifaa Tiba

  Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema ni marufuku wa mtumishi wa sekta ya afya kuhamisha vifaa hospitali  vikiwamo vya uchunguzi wa macho na atakayebainika atachukuliwa hatua za kinidhamu.

  Waziri Ummy ametoa msimamo huo leo (Ijumaa) katika Makao Makuu ya wizara hiyo Dar es Salaam wakati akipokea msaada wa vifaa huduma ya uchunguzi na kupima macho kutoka benki ya Standard Chertered.

  Amesema kumekuwa na tabia katika hospitali za mkoa na wilaya za  kuhamisha vifaa na kuvipeleka katika hospitali za binafsi na kuwataka watumishi kusimamia vyema vifaa hivyo.

  “Sitakuwa na msamaha na mtu yoyote endapo nikibaini vifaa vimeamishwa na kupeleka maeneo mengine tofauti na eneo husika,”amesema Mwalimu.

  Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Sanjay Rughani alisema vifaa hivyo zaidi ya 30 vina thamani ya zaidi ya Sh300milioni na lengo kubwa ni kupambana na upofu unaozuilika.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku