• Breaking News

  Nov 12, 2016

  Utabiri: Donald Trump Akikanyaga Afrika, Mguu wa Kwanza Kwa Dr. Magufuli

  Bara la Afrika limekuwa focus ya mataifa makubwa kutokana na utajiri wake wa maliasili ,soko kubwa la bidhaa yoyote bila ya kujali ubora wake, propaganda za kisiasa na masuala ya ulinzi na usalama . Mataifa makubwa ulimwenguni kama vile Marekani,China na Uingereza kwa kutaja machache yamejikita katika nchi za kiafrica moja kwa moja au kupitia mgongo wa mtu au taasisi fulani kwa lengo la kusongesha mbele maslai yao ya kitaifa.

  Rais anayesubiri kura kiapo cha urais wa Marekani Bwana Donald Trump inaonyesha baada ya kukalia kiti cha urais na kutupia jicho lake katika bara la Africa kuna uwezekano mkubwa kwa yeye kugongana uso kwa uso na Dr.Magufuli Rais wa Tanzania .Hii ni kwa kuwa Dr.Magufuli anachorwa kama kioo cha Africa katika mapambano dhidi ya utegemezi na Rushwa vilivyokithiri barani Africa pia anakubalika miongoni mwa waafrika na ni gumvo kwenye midia na mitandoa ya kijamii kwa sasa Africa na dunia kwa ujumla.


  Mguu wa kwanza wa Trump kwa Africa nasema utakuwa Ikulu kwa Dr.Magufuli baada kutupia macho yafuatayo:

  1. Dr.Magufuli ni Rais kutoka Africa ambaye ameonyesha kuukubali ushindi wa Trump mapema na kuonyesha kumkubali mwana mageuzi na mpambanaji huyu kwa uwazi kwa kumpongeza kupitia "tweet" kwenye akaunti yake ya Twitter mara tu baada ya matokeo ya uchanguzi kutangazwa.Trump anafanya kazi na watu wanaomkubali "regardless" ya mapungufu yake hivyo naona ata "prefer" kuanzia kwake kwanza litakapofika suala la kutua Africa.

  2.Trump ni mtu wa kazi na asiyejari maneno ya watu katika jambo ambalo lina maslai kwa Taifa la Marekani sawa sawa na Dr.Magufuli ambaye ajali maneno ya watu kwa kile ambacho anadhani kina maslai kwa Tanzania, hivyo Trump ataona atue kwanza kwa Dr.Magufuli mtu ambaye wanaweza kuongea lugha moja na kupata "insight" ya Africa ya sasa.

  3.Trump ni mtu wa maamuzi magumu hivyo naona wanaweza kuongea lugha moja na Dr.Magufuli ambaye pia ni kiongozi wa mfano hivi sasa Africa kwenye kufanya maamuzi magumu hasa ya kuwaachisha kazi wala rushwa na kuwashitaki na kuchukua hatua kali dhidi wazembe serikalini.

  4.Trump ni msema ukweli na jasiri, wala ajali huo ukweli utawaumiza vipi wengine. Ukiangalia kiundani apishani kwenye hili na Dr. Magufuli katika kugongelea misumari ya ukweli kwa mtu yeyote bila woga huku akiamini kwamba msema kweli ni mpenzi wa Mungu.Trump naamini atatamani kuonana na kiongozi mwenye sifa hii na kwa Dr.Magufuli kunasa haiepukiki atakapoligeuzia jicho bara la Afrika.


  5.Trump ameshinda uchaguzi kwa Tabu sana ,amepigana vita vya mtu mmoja, kwenye chama chake kuna watu walikuwa hata hawamsupport na kumuombea ashindwe na kumpaka matope kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii lakini Mungu si Athumani akapata Ushindi ,anashabiana na Dr.Magufuli ambaye alipata upinzani mkubwa kutoka kwa Edward Lowassa na upinzani ndani ya chama chake cha CCM na kuibuka na ushindi mwembamba, watakuwa wame"undergo" "the same Hardships and betrayal " kwenye Kampeni nafikiri watakuwa nainteresting "stories to share" hivyo Trump ataona ni vyema amuone Dr.Magufuli kwanza.

  6. Trump anampenda kufanya kazi na watu wenye uelewa mkubwa na wenye kujiamini katika wanachofanya hivyo naamini akifikiria kufanya kazi na viongozi wa Africa naona Dr.Magufuli itakuwa ndio chaguo lake la kwanza.

  7. Dr Magufuli anaongoza nchi ambayo inakubalika na kuaminiwa ,kuheshimika barani Africa kutokana na mchango wake katika kuziletea nchi nyingine uhuru na kudumisha ulinzi na usalama barani Africa hivyo Trump anaweza kutua kwanza kwa Dr.Magufuli kwa lengo la kusafisha "image" yake kwa Africa kutokana na baadhi ya matamshi yake dhidi ya baadhi ya viongozi Africa na Africa kwa ujumla ambayo yamewachukiza baadhi ya waafrica.

  8. Marais waliomtanguli (hasa G.Bush na Barack Obama) wemeonyesha "interest" ya hali ya Juu na Tanzania hasa katika kipindi cha hivi karibuni kwa kufanya ziara za kikazi nchini Tanzania nadhani kwa maslai mapana ya nchi hizi mbili au kwa hofu dhidi ya mchina ambaye ndiye mpinzani mkuu wa marekani kiuchumi kutokana na uhusiano wake wa karibu na Mtanzania na yeye kama Rais wa Marekani atakuwa hana budi kufanya kama watangulizi wake walivyofanya kwa kuendeleza uhusiano uliopo na kuuboresha hasa baada ya kuingia doa mara tu baada ya Dr.Magufuli kuingia madarakani kutokana na kufutwa kwa matokeo ya uchaguzi huko Zanzibar ambayo yalipingwa na Marekani na kupelekea Marekani kusitisha baadhi ya misaada yake kwa Tanzania kwenye siku za mwanzoni za utawala wa Dr.Magufuli.

  Nawakilisha Utabiri,

  By Article.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku