• Breaking News

  Nov 16, 2016

  VIDEO: ‘Maamuzi Niliyoyatoa Bungeni Mengine yalikuwa Hayanipendezi Hata Mimi’- Dr. Tulia Ackson


  Najua kuna watu wangu wengi wamemfahamu Naibu spika Dr. Tulia Ackson zaidi katika mkutano wa tatu wa bunge la 11 ambapo headlines nyingi ziliandikwa dhidi yake ikiwemo ishu ya wabunge wa upinzani kususia sehemu ya mkutano huo kwa madai hakuwa akitenda haki.

  Lakini ukikutana na Dr. Tulia mwenyewe ukimuuliza kama alishawahi kujutia maamuzi yoyote aliyowahi kuyafanya akiwa kwenye kiti majibu yake yatakuwa haya….


  ‘Hapana kwasababu mara nyingi nimekuwa nikifanya maamuzi kulingana na kanuni, kwahivyo maamuzi yote niliyokuwa nikifanya yaweza kuwa hayanipendezi hata mimi lakini kwa mujibu wa kanuni ni lazima yafanywe‘ –Dr. Tulia Ackson


  Aidha ukimuuliza alikuwa anajisikiaje wabunge wa upinzani kususia vikao? Dr.Tulia ameyajibu haya..>>’Wabunge kutoka ni jambo la kawaida lakini lile lilikuwa la ajabu kwa sababu wanatoka wote kwa pamoja, ningetamani wabaki lakini ni misimamo ya vyama kushughulika na wabunge wake‘ –Dr. Tulia Ackson


  ‘Wapo waliokuwa ambao walipenda kubaki lakini hawakuweza kwavile akitoka atanyang’anywa kadi yake‘ – Dr. Tulia Ackson

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku