• Breaking News

  Nov 7, 2016

  Walioficha Mapesa Uswizi Kuanza Kufuatiliwa


  Serikali ya Tanzania na Uswisi zimesaini Mkataba utakaowawezesha Maafisa wa Tanzania kwenda nchini Uswisi kufanya uchunguzi katika mabenki ya huko ili kupata taarifa sahihi za walioficha mabilioni toka Tanzania.

  Mkataba huo umesainiwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dr Augustine Mahiga na Balozi wa Uswisi nchini Florence Mattli

  Mkataba huo umesainiwa hivi karibuni wakati wa Maadhimisho ya miaka 50 ya ushirikiano kati ya Tanzania na Uswisi. Uswisi ni nchi inayosifiwa kuwa na huduma bora za kibenki huku ikiwa na sheria kali zinazowalinda wateja wake.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku