Taasisi ya Utawala Bora na Maendeleo Tanzania (Cegodeta), imeandika barua ya wazi Rais Magufuli na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, kuomba kusitisha ombi la TANESCO la kutaka kuongeza bei ya umeme ifikapo mwakani.

Mkurugenzi Mtendaji wa Cegodeta, Thomas Ngawaiya, alisema taasisi yake imepokea malalamiko kutoka kwa wananchi wakihofia kupanda kwa gharama za umeme kutasababisha kushindwa kumudu gharama za maisha.

Ngawaiya alisema matarajio ya wananchi wengi ni kuona gharama za umeme zinashuka kila siku, kutokana na utajiri wa gesi tulionao nchini.


Post a Comment

 
Top