Nov 17, 2016

Wanawake, Watoto Wakamatwa Wakidaiwa Kufunzwa Ugaidi

Kamanda Sirro
Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam imewakamata wanawake wanne na watoto wanne waliokuwa wamefichwa kwenye kambi iliyopo Kilongoni, Vikindu mkoani Pwani wakidaiwa kufundishwa jinsi ya kutumia mambo ya dini na harakati za ugaidi.

Kamanda wa kanda hiyo, Simon Sirro alisema Jeshi la Polisi kupitia kikosi kazi kinachopambana na uhalifu wa kutumia silaha na ujambazi lilifanya msako na kuwakuta wanawake na watoto hao wakiwa wamekusanywa kwenye nyumba ya mtu aliyetambulika kwa jina moja la Suleiman wakiwa wanafundishwa mambo ya dini na harakati za kigaidi.

Alisema mafunzo waliyopewa ni ya ukakamavu kama vile kareti, kungfu, judo na walikuwa wanafundishwa jinsi ya kutumia silaha za kivita na bastola.Bonyeza HAPA Kudownload Application ya Udaku Special Blog Kwenye Simu Yako

Share:

0 maoni:

Post a Comment

Trending News

Copyright © Siasa Huru | Powered by Blogger Design by JK | Blogger Theme by JR