• Breaking News

  Nov 11, 2016

  WATANZANIA 25 Wamekamatwa Nchi za Nje Kwa Kosa la Kujihushisha na Biashara za Madawa ya Kulevya

  WATANZANIA 25 wamekamatwa katika nchi za China, Brazil na Zambia kutokana na makosa ya kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya.

  Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Anthony Mavunde aliyasema hayo wakati akitoa taarifa ya hali ya dawa za kulevya nchini kwa mwaka 2015 ambayo iliwasilishwa bungeni jana.

  Akizungumza jana baada ya shughuli za Bunge za asubuhi jana, Mavunde alisema Watanzania hao 25 wamekamatwa na wanatumikia vifungo mbalimbali.

  Mavunde alisema taarifa hiyo inaonesha kuwa mwaka jana, biashara ya dawa za kulevya iliendelea kufanyika kwa kiwango kikubwa na kasi. Dawa aina ya mandrax ya kilogramu 5.1 ilikamatwa Dodoma na Ruvuma. Alisema mara ya mwisho dawa hiyo ilikamatwa mwaka 2010 nchini.

  Alisema pia bangi bado ni tatizo na kwamba hekta 50 za bangi zilichomwa huku kilogramu 161 za heroin zikiteketezwa Dar es Salaam na Tanga.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku