• Breaking News

  Nov 2, 2016

  Wateja Twiga Bancorp Wameonewa - Prof. Ngowi

  Wataalamu wa uchumi wamekosoa utaratibu uliochukuliwa na Benki Kuu ya Tanzania (BOT) wakati ikishughulikia sakata la ukosefu wa mtaji unaikabili benki ya Twiga Bancorp,

  Wamekosoa kwa maelezo kuwa hatua ya kusitisha ghafla huduma za kibenki kwa wateja wa benki hiyo haikupaswa kuchukuliwa kwa namna ilivyotekelezwa.

  Mmoja wa waliohoji utaratibu huo ni mchumi Mwandamizi na Mhadhiri wa Uchumi wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, Profesa Honest Prosper Ngowi, ambaye amesema kitendo hicho kimeleta usumbufu usio wa lazima kwa wateja wa benki ya Twiga ambao kimsingi hawahusiki na sababu zozote zilizopelekea benki hiyo kufilishika kimtaji.

  Profesa Ngowi ameenda mbali zaidi na kubainisha kuwa hatua hiyo inaweza kuwa na athari zinazofahamika kitaalamu kama 'Dominal Effect' ambapo mfumo wa kifedha nchini unaweza kupatwa na hofu ya kile kinachojulikana kama 'Run of the Bank' ambapo wateja katika benki nyingine wanaweza kupatwa na hofu ya kilichotokea kwenye benki ya Twiga na hivyo kuamua kuondoa amana zao kutoka katika benki hizo kwa mkupuo.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku