• Breaking News

  Nov 1, 2016

  Watumishi 1663 Walionufaika na Fedha za Wafanyakazi Hewa Wachukuliwa Hatua

  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angellah Kairuki amesema serikali imechukua hatua za kinidhamu dhidi ya watumishi wa umma 1663.

  Ameyasema hayo Jumanne hii bungeni mjini Dodoma kujibu swali lililotaka kujua kuhusu idadi ya watumishi hewa na hatua za serikali.

  “Hadi kufikia tarehe 25 mwezi huu wa 2016 serikali imechukua hatua za kinidhamu dhidi ya watumishi wa umma 1663 kutoka katika wizara idara zinazojitegemea,wakala za serikali sekretarieti za mikoa na mamlaka ya serikali za mitaa ambao walibainika uwepo wa watumishi hewa.”

  Akifafanua zaidi Kairuki alisema, “Kwa upande wa wizara ni watumishi wa umma 16, kwa upande wa idara zinazohitegemea na wakala wa serikali ni watumishi wa umma 9. Kwa sekretarieti za mikoa watumishi wa umma 6, mamlaka ya serikali za mitaa 1632 inayofanya jumla ya watumishi 1663.”

  “Hatua hii inajumuisha kuwasilishwa kwa masuala yanayowahusu watumishi hawa katika vyombo vya ulinzi na usalama, ambapo hadi kufikia tarehe 25 Oktoba mwaka huu jumla ya watumishi wa umma 638 wamefunguliwa mashtaka polisi,watumishi 50 wanafanyiwa uchunguzi na taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa(Takukuru), na watumishi wa umma 975 mashtaka yao yamefikishwa kwenye mamlaka zao za kinidhamu,”ameeleza.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku