• Breaking News

  Nov 16, 2016

  Waziri Kigwangalla Akamata Kiwanda Bubu cha Kutengeneza Pombe feki

  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalla, ambaye anaongoza timu ya Serikali yenye wataalamu na wanausalama, kusaka viroba feki na pombe nyingine haramu, amekamata shehena kubwa ya bidhaa hizo feki na haramu kwenye maeneo mbalimbali ikiwemo kukifuma kiwanda bubu kinachotengeneza konyagi na Smirnoff feki maeneo ya Sinza.

  Kiwanda hicho kinatengeneza vinywaji hivyo kwa kutumia 'spirit' ambayo inachanganywa na 'gongo'; spirit, gongo, chupa tupu na zilizojazwa, vizibo, vifungashio vimekamatwa.

  Polisi inawashikilia watu wawili ambao inasemekana wanafanya kazi pamoja na bwana Yusuf Abdul Kalambo, ambaye anatafutwa na polisi mpaka sasa.

  VIDEO

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku