• Breaking News

  Nov 24, 2016

  Waziri Nape Uso Kwa Uso Na Diamond Platnumz...Walichoongea Hichi Hapa

  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mheshimiwa Nape Nnauye ametembelea ofisi za Wasafi Classic Baby (WCB) zinazomilikiwa na mwanamuziki Naseeb Abdul maarufu Diamond Platnumz.

  Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Diamond Platnumz aliandika “mapema Leo ofisini kwangu, tukijadili Mawili matatu kuhusu namna ya Kuipeleka sanaa yetu kileleni na Mh: Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Mh: Nape Nauye….. Shukran sana Mkuu kwa kuendelea kutujali Wasanii, it was a great Meeting­čÖĆ”
  Adhia, baadhi ya mambo ambayo Diamond pamoja uongozi wake walijadiliana na Waziri Nnauye ni pamoja na changamoto mbalimbali zinazowakabili kama kupunjwa mapato yatokanayo na miito ya simu (Caller tunes), wizi wa kazi za wasanii, kupata eneo (Ukumbi wa Kisasa) kwa ajili ya kufanyia maonesho makubwa ya muziki, wasanii kupata elimu juu ya kulipa kodi kwa kazi zao na kuongeza kiwango cha uwiano kwa nyimbo za kitanzania zinazopigwa redioni dhidi ya nyimbo za kigeni.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku