• Breaking News

  Nov 19, 2016

  Wizi wa Watoto Wachanga Waongezeka Jijini Dar es Salaam

  Wakati kukiwa na matukio ya kikatili dhidi ya watoto ikiwamo baadhi ya wazazi kuwatupa katika majalala na vyoo, takwimu za hivi karibuni zinaonyesha watoto 44 wameibwa katika kipindi cha mwaka mmoja na miezi 10 jijini Dar es Salaam.

  Takwimu hizo zilizokusanywa na kitengo cha takwimu cha Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, zinaonyesha watoto 26 waliibwa mwaka jana na 18 mwaka huu. Pia, ilibainika kuwa watoto wengi wanaoibiwa, huibwa na wanawake ambao hawajabahatika kuzaa na huwaiba kwa minajili ya kuwalea.

   Katika mchanganuo wa takwimu hizo ilibainishwa kuwa watoto wengine huibwa hospitalini na nyumbani na baadhi katika shule.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku