• Breaking News

  Nov 2, 2016

  Yanga Wakubali Kipigo Cha Pili Msimu Huu Dhidi ya Mbeya City

  Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu soka Tanzania bara, leo November 2 2016 walishuka katika uwanja wa Sokoine Mbeya kucheza dhidi ya wenyeji wao Mbeya City katika mchezo wao wa 13 wa Ligi  Kuu Tanzania bara msimu wa 2016/2017.

  Yanga wakiwa ugenini huku wakiwa na kumbukumbu ya kipigo chao cha kwanza kutoka Stand United cha goli 1-0 September 25 2016, leo November 2 2016 wamekubali kipigo cha pili kutoka kwa Mbeya City wakiwa katika dimba la Sokoine Mbeya.

  Mbeya City wamefanikiwa kuifunga Yanga goli 2-1, magoli ambayo yalifungwa na Mwasapili dakika ya 6 na Kenny dakika 36 goli ambalo lilichukua muda kidogo refa kufanya maamuzi kutokana na wachezaji wa Yanga kuligomea, Donald Ngoma ndio alifunga goli la kufutia machozi la Yanga dakika 4 za nyongeza kabla ya kwenda mapumziko

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku