Nov 25, 2016

Yanga Wamtambulisha Kocha Mpya Rasmi..Wa Zamani Apewa Majukumu Mengine

Uongozi wa Klabu ya Yanga kupitia kwa Makamu Mwenyekiti wake, Clement Sanga amemtambulisha George Lwandamina kuwa Kocha Mkuu wa klabu hiyo katika hafla iliyofanyika Makao Makuu ya Yanga, Jwangwani jijini Dar es Salaam.

Katika hafla hiyo aliyekuwa kocha mkuu wa Yanga, Hans van Pluijm amepewa cheo cha Mkurugenzi wa Ufundi wa klabu hiyo.

Lwandamina ni raia wa Zambia ambaye alikuwa mchezaji na kocha wa timu ya taifa ya Zambia kabla ya kuikacha timu hiyo na kujiunga na Yanga ya Dar es Salaam, Tanzania.

Bonyeza HAPA Kudownload Application ya Udaku Special Blog Kwenye Simu Yako

Share:

0 maoni:

Post a Comment

Trending News

Copyright © Siasa Huru | Powered by Blogger Design by JK | Blogger Theme by JR