• Breaking News

  Dec 2, 2016

  ASKARI Mwingine Ajipiga Risasi, Afa

  Askari wa kikosi cha Suma JKT, Moses Mwita amefariki dunia baada ya kujipiga na risasi sehemu ya kifua.

  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi alisema tukio la askari kujiua limetokea leo saa 4:15 asubuhi katika kituo cha  mafuta cha BMC Mlimani kilichopo mtaa wa Bugando ambapo askari huyo alijiua kwa kutumia silaha aina ya Shortgurn.

  Msangi alisema taarifa za awali zilibaini kuwa askari huyo alionekana akizungumza na simu kwa muda mrefu kana kwamba kulikuwa na tatizo lililokuwa linamtatiza na baada ya muda alizunguka nyuma ya kituo  na kujipiga risasi kifuani hivyo kusababisha kifo chake.


  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku