• Breaking News

  Dec 25, 2016

  Hii Ndio Tabia ya Shule za Private, Wahusika Kuweni Makini

  Kuna rafiki yangu amepigiwa simu na mtoto wake anayetarajia kuanza mitihani ya kidato cha nne jumanne ya tarehe moja kwamba amtumie fedha elfu 80 kwa ajiri ya kuwahonga wasimamizi , sasa akaniomba ushauri .

  Hii tabia inataka kushamiri kwa shule hizi , na sasa ndio nimegundua kwa nini walimu wanagombania kwenda kusimamia mitihani shule za private, kwa sababu wanajua kuna fedha nyingi za bure zinapatikana huko

  Kuna baadhi ya walimu kila mwaka wanasimamia shule hiyo hiyo tu kila mwaka , na kuna baadhi ya mameneja wa shule wanahonga wataaluma ili wawapangie wasimamizi fulani fulani Tunajua ni ngumu kwa mwl kuacha hongo ya mamilioni wakati serikali imempa laki mbili tu

  Walimu wenye rekodi ya uadilifu tu ndio wapelekwe kwenye shule za private wakasimamie . Vinginevyo hizi shule ni wizi mtupu.


  By Ibesa mau/JF

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku