Dec 26, 2016

Lori Laua Padri Saa 6 Kabla ya Krismasi

Watu hao walikumbwa na mauti, baada ya lori moja la kusomba mawe, kokoto na mchanga kuparamia gari dogo aina ya Toyota Hilux, mali ya Kanisa Katoliki lililokuwa likiendeshwa na Padri Andrew Lupondya (35) wa Parokia wa Kanisa Katoliki Jimbo la Kahama mkoani Shinyanga.

Ajali hiyo ilitokea juzi saa tisa alasiri zikiwa ni saa sita kabla kuanza misa ya mkesha wa Krismasi ambayo kwa mujibu wa taratibu za Kanisa Katoliki huanza saa 3 usiku.

Watu wanne walifariki papo hapo katika eneo la tukio la Kanegele Kata ya Masumbwe wilayani Mbogwe mkoa wa Geita, katika barabara kuu kutoka Isaka kwenda Lusahunga na nchi jirani ya Rwanda, akiwamo Padri Lupondya huku watu wengine wanne wakijeruhiwa.

Bonyeza HAPA Kudownload Application ya Udaku Special Blog Kwenye Simu Yako

Share:

0 maoni:

Post a Comment

Trending News

Copyright © Siasa Huru | Powered by Blogger Design by JK | Blogger Theme by JR