• Breaking News

  Dec 25, 2016

  Vyuo vya Tanzania Vyafanya Vibaya Kwenye Takwimu za Kimataifa

  Kuna uwezekano karibu vyuo vyote vya TZA vinazalisha vilaza wa kutosha kwani kwa mujibu wa takwimu la shirika la URAP (University Ranking by Academic Perfomance) inaonyesha ni vyuo viwili tu vilivyopo kwenye top 68 ya vyuo bora afrika.

  Chuo cha kwanza ni UDSM ambacho kwa Afrika kimeshika nafasi ya 48 kati ya 68 na kidunia ni nafasi ya 1738, kikifuatiwa na chuo kikuu cha kilimo cha sokoine (SUA) kilichoshika nafasi ya 58 kati ya 68 kwa Afrika na kidunia ni 1836.

  Ambapo Makerere cha Uganda kikishika nafasi ya 9 na chuo kikuu cha Nairobi kikishika nafasi ya 25, kwa hiyo kwa nchi tatu za Afrika mashariki yaani Kenya, Uganda na Tanzania, TZ ndo ina vyuo vibovu na elimu mbovu ukilinganisha na wenzetu.

  Kwenye Takwimu za vyuo bora 30 vya Afrika za Times Higher Education(THE) Hakuna hata chuo kimoja cha kutoka Tanzania huku vyuo vya Makerere na Nairobi vikiwepo kwenye list.

  Tanzania ni kichwa cha mwendawezimu kwenye kila sekta?

  1 comment:

  1. Nothing bothers we got to go back to drawing tables n perfect it

   ReplyDelete

  Siasa

  Michezo

  Udaku